Alhamisi, Mei 18, 2017

Ronaldo avunja record iliyoshikiliwa kwa miaka 46


Mchezaji wa timu ya taifa ya Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo usiku wa jana amefanikiwa kuvunja record iliyowekwa miaka 46 iliyopita na mchezaji , Jimmy Greaves , ya Kuongoza kwa jumla ya Ufungaji wa magoli ya Ulaya na kuisadia klabu yake ya Real Madrid kunusa ubingwa wa ligi ya nchini Hispania kwa tofauti ya alama tangu 2012.
Ronaldo,mwenye umri wa miaka 31, ameifikisha Madrid kuwa kileleni baada ya kushinda goli lake la 367 katika mabao yake yote ya Ulaya, kwenye ligi kuu tano bora za Ulaya ,
 Katika mchezo huo ambao Real Madrid ilichomoza na ushindi wa magoli 4 kwa 1 dhidi ya klabu ya Celta Vigo, mchezaji huyo alitupia goli moja kati ya hayo, sasa Madrid inahitaji sare yoyote katika mchezo wake wa mwisho wa ligi wakatapo kutana na klabu ya Malaga jumapili hii , ili kujitangazia Ubingwa wa Ligi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni