Jumapili, Septemba 03, 2017

MWANZA CITY YOUTH SPORTS ACADEMY

Mwanza City Youth Sports Academy [MCYSA] ni kituo cha michezo kwa vijana wenye umri wa miaka 7 hadi 18 kilichoanzishwa mtaa wa Nyambiti,Kata ya Buzuruga,Wilaya ya ilemela katika Jiji la Mwanza kikiwa na malengo ya kugundua,kukuza na kuendeleza na kisha kutambulisha vipaji vya vijana kwenye soko la ajira.













Malengo yetu ni kuwa kituo kikubwa cha michezo sio tu ndania ya jiji la mwanza pekee bali Tanzania nzima na Afrika kwa ujumla.Japo kwasasa vijana wengi tulionao ni kutoka kata ya Buzuruga na kata za jirani kama Mabatini na Nyakato lakini mpango uliopo ni kuwafikia vijana wa jiji zima la Mwanza na baadae Tanzania nzima.

Mwanzo umekuwa mgumu na changamoto ni nyingi mno,hasa changamoto ya viwanja vya michezo na  vifaa vyake kama vile Mipira na Jezi lakini pia vifaa vya kufanyia mazoezi kama Bips na Cones kwa michezo ya Soka,Pete,Kikapu na Wavu.

Tunaomba msaada wako katika kufanikisha lengo letu la kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana ambao ndio Taifa la kesho ili waweze kutumia vipaji vyao kujiajiri na kupata vipato kwaajili yao,familia zao na kuleta mabadiliko chanya katika jamii na Taifa kwa ujumla.